TUKIKUZE KISWAHILI
- Kiswahili lugha yetu, tuitunze kwa mapenzi Tujifunze kwa wenzetu, wachina siwamalizi Huu ni wajibu wetu, kwa nguvu na tukienzi Tusimame himahima, lugha yetu kjuikuza.
- Walimu na Wanafunzi, sote na tusonge mbele Na tusifanye ajizi, tukipigie kelele Tukinene waziwazi, kiswahili chende mbele Tusimamae hima hima, lugha yetu kukikuza
- Tusifanye masihara, kiswahili kupuuza Tutaingia hasara, tukija kukipoteza Ila takuwa imara, sisi kukiendeleza Tusimamae hima hima, lugha yetu kuikuza.
Mhariri;WANJE MUSSA MAKAME