KISWAHILI DUNIANI
Alhamisi, 4 Januari 2018
TUKIKUZE KISWAHILI
- Kiswahili lugha yetu, tuitunze kwa mapenzi Tujifunze kwa wenzetu, wachina siwamalizi Huu ni wajibu wetu, kwa nguvu na tukienzi Tusimame himahima, lugha yetu kjuikuza.
- Walimu na Wanafunzi, sote na tusonge mbele Na tusifanye ajizi, tukipigie kelele Tukinene waziwazi, kiswahili chende mbele Tusimamae hima hima, lugha yetu kukikuza
- Tusifanye masihara, kiswahili kupuuza Tutaingia hasara, tukija kukipoteza Ila takuwa imara, sisi kukiendeleza Tusimamae hima hima, lugha yetu kuikuza.
Mhariri;WANJE MUSSA MAKAME
Jumanne, 2 Januari 2018
Alhamisi, 28 Desemba 2017
Kiswahili duniani kimepata watumiaji wengi kutokana na urahisi wake katika mazungumzo.Lugha hii inatumika katika vyombo vya habari vya kimataifa mfano BBC Swahili na Deutsche welle pia hutumika katika mikutano ya wakuu wa nchi za Afrika [AU].Pia Kiswahili hutumika katika vyuo vikuu mbali mbali duniani mfano Marekani.
Jumapili, 24 Desemba 2017
KISWAHILI
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)